International news

Marekani wamuota Ben Carson White House..

Dr. Benjamin Carson akihutubia katika moja ya mikutano mikubwa ya Kisiasa iliyoandaliwa na Conservative"
Dr. Benjamin Carson
Ile hali ya sintofahamu katika kujua nani atakuwa mrithi wa kiti cha uraisi wa Taifa hili kubwa la Marekani inazidi kuwafanya wamerakani kumwota zaidi Daktari bingwa duniani mwenye mikono iliyobarikiwa kutibu magonjwa yanahusu ubongo na akili (The Gifted Handed idol)  Ben Carson.                                                         Aidha Ben carson anapewa nafasi kubwa zaidi na watu weusi na pia inaonekana wazi wazi kwamba hata wale wafuasi wa "Conservatives" wanaonekana kumuunga mkono ikiwemo Rais Barack Obama. Carson anahusihwa na maandalizi ya mbio za uraisi kufuatia kutokea mara kwa mara katika vyombo vya habari na pia katika mijadala mikubwa akitoa misimamo yake kuhusu masuala mbali mbali yanayoikumba Marekani. Kuonekana huko katika majukwaa ya kisiasa akizungumza maswala yanayoigusa marekani hasa makosa yaliyofanywa na serikali ya sasa na kulezea jinsi gani makosa hayo yanapaswa kutatuliwa kumemfanya Carson kuwa mwiba kwa Democratic na hivyo daktari huyu bingwa kupewa nafasi kubwa ya kuingia ikulu baada ya Obama.                                    Hata hivyo kama kweli carson ana nia madhubuti ya kuwania uraisi wa Marekani wakati huu unaonekana kuwa sahihi zaidi kufuatia kustaafu kwa Carl Levin (D) senetor wa Michigan (alipozaliwa Ben Carson)  alietangaza kutogombea tena baada ya kuisha kwa muhula huu wa uongozi. Hivyo ni nafasi sahihi sasa kwa Carson kuwania kiti hicho na endapo atashinda basi atajinyakulia umaarufu mkubwa pamoja hivyo kuongeza nguvu katika kampeni za uraisi..                                                                                                                                             Kila la Kheri  Dr. Ben....

                                                                                                                                            

Kenya Kwa Pamba Moto!!! Polisi TISA wapoteza maisha
Askari wa Jeshi la ulinzi wakiwa Katika eneo lililoshambuliwa.


Zoezi la kupiga kura Nchini Kenya limekamilika huku  kukiwa na dosari kadhaa ikiwemo Kuchelewa kufungua vituo pamoja na foleni ndefu katika kuelekea kupiga kura. Aidha imeripotiwa kuwa watu takribani 15 wamepoteza maisha Kufuatia milipuko pamoja na mashambulizi yaliyoelekezwa kwa Polisi karibu kabisa na maeneo ya kupigia kura. Inasemekana Kwamba polisi wapataoTisa wamepoteza maisha pamoja na washambuliaji Sita hivyo kufanya jumla ya watu wote waliopoteza maisha katika tukio hilo kuwa 15. Hata hivyo  Katika siku ya Juma Pili iliripotiwa kuwepo kwa milipuko kadhaa kaskazini mwa Kenya. 
Raila Odinga moja ya wagombea akipiga Kura Yake
   Matokeo ya awali ya uchaguzi huu yameanza kutolewa na tume ya uchaguzi huku Kenyata akiendelea Kuongoza Kura hizo za awali kwa takribani ya asilimia kumi (10%). Hata hivyo Matokeo haya ni ya wali sana kwani jumla Ya waliopiga kura ni zaaidi ya raia Milioni 13 hivyo inategemewa kuwepo kwa mchuano mkali Kati ya Uhuru Kenyatta na Raila Odiga katika kuwania Kiti cha Uraisi.
               Hata hivyo Kinyanganyiro hicho kinaonekana kuwa kigumu zaidi kufuatia Katiba Kuhitaji Mshindi wa Kiti hicho lazima awe ameshinda Kwa idadi Kubwa ya kura katika "County" 24 kati ya County zote 47 na kama ikitokea mshindi ameshindwa kufikia asilimia Hiyo (5I% ya Ushindi wa COUNTY) basi uchaguzi huo utaingia Raundi ya pili mabapo washindi wa wili Wa juu watachuana Tena April Mwaka Huu.

                                                                                                                                       

 Siku ya Mwisho ya Papa Kuwepo Vatican

 
Siku Ya Mwisho Kwa Papa Benedict 16 Kuwepo Vatican, Asema Atamtii Mrithi wake. Papa Benedict 16 (miaka 85) awaaga rasmi waumini wa kanisa Katoliki duniani Kote. Akiwa katika harakati za Kuondoka Vatican Papa Benedict amewaaga makardinali waliohudhuria tukio hilo na kuahidi kumtii mrithi wake. hata Hivyo amesema Kwamba ana imani kwamba Mungu atawaongoza makadinali hao kumchagua mtu hasa atakaefaa kuwa mrithi wake. .











No comments:

Post a Comment