Friday, January 3, 2014


Breaking News! Breaking News! 
Mfanya biashara Kariakoo apigwa risasi kweupee  na kisha majambazi  kupora Mabegi mawili yaliyojaa fedha ...

Mfanyabiashara mmoja (Jina Halikufahamika) Mwenye asili ya Asia ameshambuliwa na majabazi (majira ya saa 12 Kasoro jioni )kwa kupigwa risasi katika paji la uso wake na kisha majambazi hao kutoweka na mabegi mawili yaliyoojaa fedha.
Damu ya Mfanyabiashara huyo ikiwa imetapakaa katika gari lake baada ya kupigwa risasi na majambazi waliompora kiasi kikubwa cha fedha na kutoweka.

Hata hivyo haikujulikana kwa haraka ni kiasi gani cha fedha ambacho kilikuwemo katika mabegi hayo. Wakiongea na mwandishi wetu baadhi ya mashuhuda wa tukio walidai kuwa majambazi hao walikuwa  watatu na mmoja alikuwa na bunduki aina ya SMG. 
Raia wakishangaa mwili wa mfayabiashara huo ukiondolowa na polisi
           Wakielezea tukio hilo baadhi ya wafanyabiashara wengine katika maeneo hayo ya mtaa wa Lindi na Kongo (Kariakoo) walidai kwamba Mfanyabiashara huyo alitoka na kufunga duka lake huku akiwa na mabegi mawili na Mashine ya kutolea Risiti ya EFD na kuelekea katika gari lake dogo aina ya Suzuki Carry na Ghafla walitokea watu wawili waliokuwa katika pikipiki na mmoja wa tatu alikuwa amesimama pembeni kidogo na gari hiyo na kisha kuelekea moja kwa moja katika gari hiyo na kumpiga risasi mfanya biashara huyo aliyekuwa akijiandaa kuondosha gari lake.

         
Mfanya biashara apigwa risasi Kariakoo
Askari wakiliondoa gari la mfanya biashara huyo katika eneo la tukio
''Niliona watu kama wanagombania begi hivi ghafla nikasikia mlio wa risasi  na kisha nikaona pikipiki mbili aina ya boxer zikija kwa kasi kutokea upande wa mtaa wa gerezani na kisha  mlio wa pili wa risasi ulikika tena, nahisi ndio uliokuwa umemlenga yule "muhindi" na baada ya hapo kitendo kama cha dakika mbili hivi wale jamaa wakapokezana lile begi na kisha kupiga risasi nyingine juu basi hapo wote tukaanza kufunga maduka yetu na wale majambazi wakatoweka kirahisiii"
EFD machine ikiwa katika gari la mfanyabiashara aliyepigwa risasi leo jijini Dar es Salaam

Sehemu  ya fremu inayosemekana kuwa ni Duka la
 Mfanyabiashara aliyepigwa Risasi Leo majira ya saa 12 jioni
Hata hivyo baadhi ya watu wamelaumu utaratibu wa wafanya biashara wengi wa kariakoo kuhifadhi fedha nyingi katika maduka na badala yake wamewataka wafanya biashara hao kutafuta mbinu mbadala itakayowaezesha kuweka fedha na mali zao salama kabisa ikiwa ni pamoja na kutumia huduma za kuhamisha fedha kwa kutumia mitandao, cheque, na hata credit card kuliko Cash kwani imekuwa kawaida kwa mtukio haya kujirudia eleo hili la Kariakoo.

No comments:

Post a Comment