Sunday, June 19, 2011

Mtoto wa Afrika

Picha by guardian angeltz
Tarehe 16 juni ni siku ya mtoto wa afrika ambapo watoto barani Afrika hupata fursa ya kukaa pamoja na kudai kuhoji na kuomba haki zao za msingi. Msingi wa siku kuu hii ni kuwapa nafasi watoto ya kueleza hisi zao na kudai haki zao ikiwa kama moja ya njia ya kuwajengea watoto misingi ya maisha bora. Watoto wana haki nyingi ikiwemo Haki ya kupata elimu, matibabu na huduma nyingine muhimu , Haki ya kucheza, haki ya kupewa malezi bora hali kadhalika watoto wana haki ya ki msingi kabisa ya kupewa upendo na familia zao. lakini katika hali ya kushangaza suala hili la watotot wa mitaani limezidi kuwa tatizo kubwa barani afrika hasa katika nchi masikini kama Tanzania na kadhalika. Wito wangu kwa jamii ni kuliangalia upya suala hili na kuchukua hatua madhubuti ili kuwasaiidia watoto hao. Rafiki zangu na watanzania wenzangu watoto hawa wa mitaani wanaishi maisha magumu sana huko kwa kukosa mahitaji muhimu kama mavazi makazi na pia malazi. Watoto hawa wa mitahani wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya viruhsi vya ukimwi, kujiingiza katika uhalifu pamoja na mambo mengine mengi mabaya ikiwa ni pamoja na udhalilishaji wa kijinsia kama vile Kubakwa na Ulawiti. Inasikitisha sana ndugu zangu! Watoto Hawa ni watoto wetu ni watoto wa Afrika ni Ndigu zetu lakini pia ni Nguvu kazi ya taifa, Ninachoamini mimi tatizo la watoto wa mitaaani linatatulika kama tukiwa makini na tukiamua kwa dhati kabisa kulitokomeza. Hakuna mtoto wa mtaani hata mmoja anaye furahia maisha anayoishi ila ndio hivyo tena hana pa kwenda. Sababu kuu ya kuongezeka kwa wimbi la watoto wa mitaani kwanza kabisa ni Gonjwa la ukimwi ambapo watoto hawa huachwa yatima na hivyo kuamua kuingia mtaani kujitafutia chochote. Lakini pia UZEMBE wa badhi ya wazazi huchangia katika kuongeza wimbi la watoto hawa kwa baadhi ya wazazi wamekuwa hawawajali watoto wao na kuwatelekeza bila kuwapatia mahitaji muhimu. Suala lingine ni swala Talaka wazazi wanapo talikiana watoto hubaki katikati na kushindwa kupata maamuzi wapi pa kufuata sasa katika hili wazazi hawa wasipokua makini watoto wanaweza wakajikuta wanapoteza muelekeo na kujidumbukiza katika bwawa la watoto wa mtaani. Sasa  cha kufanya ni kuamua kwa pamoja kusimamia kwa pamoja huku tukishirikiana na serikali kutokomeza na kukomesha tabia hii ya kinyanyasaji ya wazazi kuwatelekeza watoto wao kwa kuwashughuliki ipasavyo wale watakao fanya hivyo. Lakini PIA Serikali Ibuni sera madhubuti ya kuwaondoa watoto hawa mitaani aidha kwa kufungua training centers ambapo watoto hawa watapatiwa elimu ya ujasiria mali na uraia ili wawe asset muhimu na nguvu kazi kwa taifa hili. kwa kufanya hivyo naamini ipo siku tatizo hili litapotea na kubaki historia.
                                                                           
  Mungu ibariki Tanzania Mungu Mbariki Mtoto wa Afrika

No comments:

Post a Comment