KANAL MUAMAR GADDAFI: Gadaffi ni nguzo pekee ya umoja wa afrika ambayo kwa sasa mataifa mbali mbali ya ulaya yanatumia kivuli cha haki za binadamu kutaka kumng'oa? Nikiwa kama mwanaharakati muafrika mwenye upendo na bara langu pamoja na wafrika wenzangu naguswa mno na machafuko Yaliyoandaliwa yanayoendelea Libya. wanaomshambulia Gaddafi kwa sasa hawana hoja ya msingi ya kutueleza kwa nini na ni sababu zipi zilizowapa mamlaka ya kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine tena nchi huru ambayo inaendeshwa na jamhuri. kinacho nisikitisha zaidi ni kwamba hao Wababe wanaomshambulia Gaddafi ni walle wale wababe tuliowaona wakimshambulia Saddam Hussein kwa kisingizio cha kumiliki silaha za maangamizi.Naitaka dunia ielewe kuwa Africa ni Bara lenye umoja wake uitwao "AU" ambao ndio haswa wenye jukumu la kushughulikia matatizo yote yanaihusu Afrika, Cha kushangaza hawa wanaojiita umoja wa kujihami ambapo hakuna hata nchi moja ya Afrika ni mwanachama wanakurupuka na kumvamia Gaddafi. Tumeona maandamano yakiendelea Londoni hivi karibuni kuhusu ugumu wa maisha , mshahara mdogo pamoja na gharama za juu, kinachonishangaza ni kwamba hayo mataifa wala hayaangalii ni jinsi gani ya kuwasaidia rai wao wanakimbilia kwa raia wa wenzao... Wito wangu kwa mataifa ya afrika ni kuungan ana tuwe na sauti moja ambayo itawaondoa hawa maharamia wa kizungu wasiendelee kuwaumiza ndugu zetu. Hakuna ugaidi kwa sasa Bali NATO ndio Magaidi wa Kuuu...
No comments:
Post a Comment